Home / Machapisho / Udahili

BlueSky Secondary School Yafungua Udahili wa Form One 2027

BlueSky Communications 22 Aug 2026 2 views
BlueSky Secondary School Yafungua Udahili wa Form One 2027

BlueSky Secondary School, Kigoma, imetangaza rasmi kuanza kwa udahili wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2027. Wazazi na walezi wanakaribishwa kuwasilisha maombi mapema.

BlueSky Secondary School imefungua rasmi nafasi za masomo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2027.

BlueSky ni shule ya bweni kwa wavulana na wasichana, inayotoa elimu bora ya Sekondari pamoja na Mkondo wa Amali. Mfumo wetu wa elimu unaunganisha maarifa ya darasani, maadili, nidhamu, uongozi na stadi za vitendo zinazomwandaa mwanafunzi kwa maisha na dunia ya kazi.

Kwa nini uchague BlueSky Secondary School?

Shule ina mazingira salama na tulivu ya kujifunzia, walimu wenye uzoefu, huduma ya bweni, maji ya kutosha na umeme wa uhakika. Wanafunzi pia hupata fursa ya kujifunza vocational skills na entrepreneurship skills kwa ajili ya kujenga uwezo, ubunifu na kujitegemea.

Ada na michango yote ni TZS 1,600,000 kwa mwaka. Malipo yanaweza kufanyika kwa awamu nne ili kuwasaidia wazazi na walezi kupanga gharama za elimu kwa urahisi.

Shule pia inaendesha programu ya Pre-Form One inayolenga kuwaandaa wanafunzi kitaaluma, kimaadili na kimazingira kabla ya kuanza rasmi masomo ya sekondari.

Wazazi na walezi wanashauriwa kutuma maombi mapema kwa sababu nafasi ni chache. Maombi ya awali yanaweza kufanyika kupitia website rasmi ya shule. Joining Instructions na fomu nyingine muhimu zinapatikana katika Downloads Centre ya website.

BlueSky Secondary School ipo Mkoa wa Kigoma, kilomita 35 kutoka Manispaa ya Kigoma/Ujiji, kando ya barabara ya Kigoma–Kasulu, jirani na Seminari ya Iterambogo, Kata ya Matendo.

Kwa mawasiliano zaidi, piga simu +255 748 339 881 au +255 663 583 527. Unaweza pia kutuma barua pepe kupitia [blueskykigoma@gmail.com](mailto:blueskykigoma@gmail.com).

BlueSky Secondary School — Learn for Life.